Mourihno akomaa kwa Griezmann

Muktasari:

Bosi huyo wa Old Trafford anataka mrithi sahihi wa Zlatan Ibrahimovic pamoja na mchezaji wa kuziba pengo la Wayne Rooney msimu ujao.

London, England. Jose Mourinho amezamilia kuhakikisha anamsajili mshambuliaji Antoine Griezmann atakayeighalimu Manchester United pauni 86milioni.
Bosi huyo wa Old Trafford anataka mrithi sahihi wa Zlatan Ibrahimovic pamoja na mchezaji wa kuziba pengo la Wayne Rooney msimu ujao.
Nyota huyo wa Atletico Madrid, Griezmann inavyoonekana sasa ni suala la muda tu kabla ya kusaini mkataba kwa majibu wa gazeti la Manchester Evening News.
Griezmann (26), ni rafiki wa karibu wa kiungo wa Man United, Mfaransa Paul Pogba.
Mbali ya mchezaji huyo, Mourinho pia amekuwa akimfuatilia kwa karibu mshambuliaji wa Everton, Romelu Lukaku.