Mrwanda: Sina mipango ya kuwa kocha

Muktasari:

  • Mrwanda ni miongoni mwa wachezaji matajiri Ligi Kuu, alisema kwa kipindi cha miaka 16 aliyocheza soka amefanikiwa kutengeneza miraji mbalimbali.

Dar es Salaam. Nyota wa zamani wa Simba na Yanga, Danny Mrwanda amesema atakapostaafu kucheza soka hana mpango wa kujifunza ukocha kwa sababu ana shughuli nyingine za kufanya.

Mrwanda ni miongoni mwa wachezaji matajiri Ligi Kuu, alisema kwa kipindi cha miaka 16 aliyocheza soka amefanikiwa kutengeneza miraji mbalimbali.

"Nashukuru kwani tangu nimeanza kucheza soka nimepata mafanikio makubwa. Vipo vitu ambavyo nikivitazama naona kabisa kama siyo soka nisingevipata," alisema Mrwanda ambaye anaendelesha gari aina ya Prado.

"Bado nina miaka kadhaa ya kucheza soka, pindi nikimaliza kucheza soka sitakuwa na mpango wa kufanya kazi ya ukocha, nafikiria zaidi kuendeleza miradi yangu," alisema Mrwanda.