Nape aweka hadharani kamati ya Serengeti Boys

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Nnauye

Muktasari:

  • Kamati hiyo inajumuishwaa wanahabari, viongozi wa kampuni na vyombo vya habaru na wasanii.
  • Waziri Nape amesema jukumu kubwa la kamati hiyo nii kuhakikisha wananchi wanashirikishwa kwenye maandalizi ya timu hiyo.

Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Nnauye ametangaza kamati ya watu 10 itakayohusika kutoa hamasa kwa Watanzania ili kusidia maandalizi ya timu ya vijana ya Serengeti Boys.

Kamati hiyo inajumuishwaa wanahabari, viongozi wa kampuni na vyombo vya habaru na wasanii.

Waziri Nape amesema jukumu kubwa la kamati hiyo nii kuhakikisha wananchi wanashirikishwa kwenye maandalizi ya timu hiyo.

"Tumedhamiria kuona timu hii inafanya maandalizi makubwa na nimeongea na Malinzi asubuhi hii yuko Morocco akiweka sawa kambi ya vijana,"amesema Nape.

Kamati hiyo itakuwa chini ya uenyekiti wa mwanahabari mkongwe Charles Hillary na katibu wake atakuwa Mwesigwa Selestine.

Wajumbe wa kamati hiyo nii Beatrice Singano, Ruge Mutahaba, Maulid Kitenge, Erick Shigongo, Hassan Abbas, Hoyce Temu na wanamuziki Ally Kiba na Diamond Platnumz.

Serengeti Boys itacheza fainali za vijana Afrika baada ya kushinda rufani yake dhidi ya Congo-Brazzaville iliyomchezesha mchezaji Langa Lesse Bercy ambaye umri wake ulizidi miaka 17.