Newcastle, Chelsea zararuana kwa Caballero

Muktasari:

Caballero amekuwa akihusishwa kujiunga na Chelsea na anatarajiwa kuondoka kwenye dimba la Etihad mkataba wake utakapomalizika msimu wa kiangazi.

Klabu ya Newcastle inapigana vikumbo na Chelsea kwenye mbio za kumuwania kipa wa Manchester City, Willy Caballero.

Caballero amekuwa akihusishwa kujiunga na Chelsea na anatarajiwa kuondoka kwenye dimba la Etihad mkataba wake utakapomalizika msimu wa kiangazi.

Hata hivyo, Manchester City imemkomalia kuendelea kubaki klabuni hapo baada ya kipa Ederson kwenda kujinga na klabu ya Benfica.

Ndoto za Antonio Conte ilikuwa ni kumsajili Caballero kwenye dimba la Stamford Bridge ili kumuongezea nguvu Thibaut Courtois kwa lengo la kuziba nafasi ya Asmir Begovic aliyejiunga na Bournemouth.