Samatta atupwa nduguze Europa Ligi

Muktasari:

Katika ratiba ya Europa Ligi iliyopangwa mjini Nyon imeonyesha timu ya Samata iliyofuzu kwa hatua 16 kwa kuitoa FC Astra ya Romania kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2 itakuwa ugenini kucheza na ndugu zao wa Gent.

Nyon, Uswisi. Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania na Genk, Mbwana Samatta ataanza harakati za kusaka kufuzu kwa robo fainali Europa Ligi kwa kuivaa Gent katika mchezo wa hatua ya 16 bora.
Katika ratiba ya Europa Ligi iliyopangwa mjini Nyon imeonyesha timu ya Samata iliyofuzu kwa hatua 16 kwa kuitoa FC Astra ya Romania kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2 itakuwa ugenini kucheza na ndugu zao wa Gent.
Endapo Genk itafanikiwa kufuzu kwa robo fainali basi Samata atakuwa Mtanzania wa kwanza kufuzu kwa hatua hiyo ya mashindano hayo ya pili kwa ukubwa barani Ulaya.
Katika ratiba hiyo timu pekee ya England iliyobaki katika mashindano hayo Manchester United imepangwa kucheza na Rostov na mechi ya kwanza itafanyika Russia.
Nayo Copenhagen itacheza na Ajax wakati Olympiacos wataivaa Besiktas huku APOEL itaikaribisha Anderlecht nayo Celta Vigo watajiuliza kwa Krasnodar.
Miamba ya Ufaransa, Lyon wataonyeshana kazi na Roma wakati Schalke wataonyeshana kazi na ndugu zao wa  Borussia Monchengladbach