Simba ‘yashikwa’

Muktasari:

Sare hiyo inaifanya Simba kufikisha pointi nne sawa na Azam, lakini zikitofautiana kwa idadi ya mabao ya kufunga.

Simba imelazimishwa sare ya bila kufungana na JKT Ruvu hivyo kuipisha Azam kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya jana kuichapa Majimaji mabao 3-0.

Sare hiyo inaifanya Simba kufikisha pointi nne sawa na Azam, lakini zikitofautiana kwa idadi ya mabao ya kufunga.

Matokeo hayo ya Simba yanatoa mwanya pia kwa mahasimu wao Yanga kujipanga zaidi kwani mabingwa hao watetezi wanaanza kutupa karata yao ya kwanza leo kwa kucheza na African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa.

Simba ilianza mchezo huo kwa kasi kwa Laudit Mavugo kukosa bao dakika ya nane ya mchezo baada ya kuachia shuti kali lililodakwa na kipa wa JKT Ruvu, Said Kipao huku Maguvo akikosa tena bao baada ya faulo aliyopiga dakika ya 12 kupaa nje kidogo ya lango.