Wagombea TFF wazidi kumiminika

Muktasari:

Nyamlani sasa atavaana na Jamal Malinzi anayetetea nafasi yake, Imani Madega, Wallace Karia, Fredrick Masolwa huku Ally Mayai naye akitajwa kuwa angechukua fomu muda wowote wakati Makamu wa Rais mpaka sasa walikuwa ni Mulamu Ng'ambi, Michael Wambura na Geofrey Nyange 'Kaburu'.

Mpaka leo Jumapili mchana wagombea zaidi ya 45 wamechukuwa fomu za kuwania nafasi mbalimbali ndani ya Shirikisho la Soka nchini (TFF), huku Athuman Nyamlani akichukua fomu ya kuwania nafasi ya urais.

Nyamlani sasa atavaana na Jamal Malinzi anayetetea nafasi yake, Imani Madega, Wallace Karia, Fredrick Masolwa huku Ally Mayai naye akitajwa kuwa angechukua fomu muda wowote wakati Makamu wa Rais mpaka sasa walikuwa ni Mulamu Ng'ambi, Michael Wambura na Geofrey Nyange 'Kaburu'.

Nyamlani ambaye aliwahi kuwa makamu wa rais katika uongozi wa Rais Leodeger Tenga, amechukuwa fomu hiyo leo pamoja na wajumbe watano ambao ni Abdallah Mussa, Peter Steven, Said Tulliy, Ally Musa na Mussa Kisoki.

Wajumbe waliochukuwa jana Jumamosi ni Salum Chama, Ephraim Majinge, Elias Mwanjala, Saleh Alawi, Kaliro Samson, Vedastus Lufano, Kenneth Pesambili, Mbasha Matutu, Samweli Daniel, Dunstan Mkundi, Athuman Kambi, Shafii Dauda, Golden Sanga na Charles Mwakambaya.

Wengine ni Benista Rugola, Thabit Kandoro, Goodluck Moshi, James Mhagama, Hussein Mwamba, Sarah Chao, Issah Bukuku, Stewat Masima, Emmanuel Ashery, Abdul Sauko, Musa Sima, Stanslaus Nyongo, Ayoub Nyenzi, John Kadutu, Baraka Mazengo, Khalid Mohamed, Cyprian Kayuva na Saleh Abdul.