Washiriki 3,000 kushiriki Mbio za Mount Meru

Muktasari:

  • Mratibu wa mbio hizo Alfred Nicolaus alisema mashindano ya mwaka huu yatakuwa na idadi kubwa ya washiriki tofauti na miaka ya nyuma na hii itasaidia kutimiza lengo waliloliweka ikiwa pamoja na kutangaza vivutio vya kitalii vinavyopatikana Mkoani Arusha hasa mlima Meru.

Arusha: Wanariadha 3000 wanategemea kushiriki mashindano ya  Mount Meru half Marathoni yatayofanyika Oktoba mosi mwaka huu.

Mratibu wa mbio hizo Alfred Nicolaus alisema mashindano ya mwaka huu yatakuwa na idadi kubwa ya washiriki tofauti na miaka ya nyuma na hii itasaidia kutimiza lengo waliloliweka ikiwa pamoja na kutangaza vivutio vya kitalii vinavyopatikana Mkoani Arusha hasa mlima Meru.
Mashindano hayo ya nusu marathon yameyagawa kulingana na makundi ya wanaridha watakaoshiriki mashindano ya mbio ndefu na kundi la pili ni wale wanaoshiriki mashindano ya mbio fupi yaani ya kujifurahisha hasa wazee na watoto.

 “Bado kuna changamoto ya kuwapata wanariadha wanawake hata ukiwapata wengi wanakuwa wa kushiriki mbio fupi, hivyo kuwapata ni hadi katika vyuo na shule, japo JKT, na jeshi la magereza na polisi ndio wanajitahidi kuzalisha wanariadha wanawake.

“Maandalizi yanakwenda vizuri tukishirikiana na chama cha riadha mkoa Arusha (ARAA), lengo ni kuibua vipaji vya wanariadha, kutangaza vivutio vya kitalii vile vile kupiga vita maambukizi ya ukimwi.” alisema Nicolaus.