Yanga, Simba zapigwa mkwara

Muktasari:

  • Mara kadhaa wachezaji wa timu hizo, kipimo chao kikubwa ni kwenye mechi za mahasimu na baadhi ya mechi kubwa za Ligi Kuu, kwamba mchezaji anapoharibu, hupoteza namba na imani kwa mashabiki na viongozi.

Dar es Salaam. Viongozi na mashabiki wa klabu za Simba na Yanga wanasifika kwa kuwakuza wachezaji, lakini wamekuwa chanzo cha kushuka viwango vya nyota wao katika klabu zao.

Mara kadhaa wachezaji wa timu hizo, kipimo chao kikubwa ni kwenye mechi za mahasimu na baadhi ya mechi kubwa za Ligi Kuu, kwamba mchezaji anapoharibu, hupoteza namba na imani kwa mashabiki na viongozi.

Baadhi ya wachezaji walioonja machungu ya mashabiki na viongozi wa timu hizo kipa wa Yanga, Ally Mustafa ‘Barthez’, ambaye aliingia Yanga kwa mguu mzuri baada ya kuiongoza kutwaa ubingwa wa Kagame mwaka 2013 na Ligi Kuu msimu wa 2014/2015, lakini baadaye alituhumiwa kufungwa magoli ya kizembe na Simba.

Barthez alituhumiwa na mashabiki wa Yanga kuwa alifungwa mabao ya kizembe katika sare ya mabao 3-3 baina ya Yanga na Simba, Oktoba 2013, katika ushindi wa bao 1-0 ambao Simba waliupata dhidi ya Yanga, Machi 2015 na katika sare ya bao 1-1 kati ya timu hizo, Oktoba mwaka jana.