Yanga yaionya Ashanti isirudie

Winga wa Yanga, Simon Msuva (kushoto) akipiga krosi mbele ya beki wa Ashanti United, Peter Mutambuzi katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam jana. Yanga ilishinda 4-1. Picha kwa hisani ya Bin Zubeiry

Muktasari:

  • Matokeo hayo yanaiweka Yanga pazuri kusogea mbele hatua ya 16 bora na hata kutetea ubingwa wake ilioutwaa mwaka jana.

Dar es Salaam.  Mabingwa wa Kombe la FA, Yanga wamejipigia Ashanti United mabao 4-1 katika mchezo wa upande mmoja kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Matokeo hayo yanaiweka Yanga pazuri kusogea mbele hatua ya 16 bora na hata kutetea ubingwa wake ilioutwaa mwaka jana.

Hata hivyo, pamoja na Yanga kushusha kikosi kamili na kushinda mchezo huo, ulikosa kasi na msisiko sehemu kubwa ya mchezo.

Yanga ilipata bao la kwanza dakika ya 19 lililofungwa na Amiss Tambwe akimalizia pande la Saimon Msuva kabla ya Thaban Kamusoko kufunga ‘bao la mwendo kasi’ dakika ya 36, ikiwa ni shuti la umbali wa mita 30.