Mkapa ataka Serikali isimamie uzalishaji umeme jua

Muktasari:

Rais mstaafu Mkapa amesema umeme huo utasaidia kuepukana na uharibifu wa mazingira


Dar es Salaam. Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa amesema uzalishaji wa umeme jua hapa nchini utachangia kuepukana na changamoto ya uharibifu wa Mazingira.

Kauli hiyo ameitoa leo Juni 19, 2018 jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa Kitabu cha Mafunzo ya Umeme wa Jua uliofanyika Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech).

"Kinachohitajika kwa sasa ni kuweka mipango madhubuti na kuitekeleza, lakini ili kufanikisha hilo, tunahitaji taasisi muhimu za Serikali kama Costech kusimamia mipango hiyo kwa kushirikiana na wabia wa maendeleo na wataalamu mbalimbali kutoka serikalini na sekta binafsi,"amesema Mkapa.

Mkapa amesema Sera ya Taifa ya Nishati ya Mwaka 2015, inaeleza wazi umuhimu wa nishati ili kufikia uchumi endelevu na usioharibu mazingira.