Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkoa mpya wa kipolisi kuanzishwa Rufiji

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba

Muktasari:

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amelieleza Bunge leo (Jumanne) katika hotuba yake ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2017/18.

Dodoma. Serikali imetangaza kuanzisha mkoa mpya wa kipolisi katika wilaya za Mkuranga, Kibiti,  Rufiji na Mafia ili kuimarisha usalama katika maeneo hayo.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amelieleza Bunge leo (Jumanne) katika hotuba yake ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2017/18.

Nchemba amesema mkoa huo utaitwa Mkoa wa Kipolisi Rufiji.

Kibiti kumekuwa na matukio mbambali ya mauaji ambayo yamegharimu maisha ya baadhi ya wananchi.