Mkurugenzi Gairo amshusha cheo mhandisi wa wilaya

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Gairo, Agnes Mkandya

Muktasari:

“Kwa sasa nimemshusha cheo mhandisi wa wilaya kutokana na kutojituma kwake katika masuala ya ujenzi na taarifa nimeshapeleka mkoani,”amesema Mkandya leo wakati akizungumza na Mwananchi.

Gairo. Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Gairo, Agnes Mkandya amemshusha cheo mhandisi wa wilaya hiyo, Gabriel Mamilo kutokana na kutosimamia ipasavyo miradi mbalimbali ya ujenzi hasa barabara na madaraja.

“Kwa sasa nimemshusha cheo mhandisi wa wilaya kutokana na kutojituma kwake katika masuala ya ujenzi na taarifa nimeshapeleka mkoani,”amesema Mkandya leo wakati akizungumza na Mwananchi.

Mkandya amesema kama mtendaji mkuu wa halmashauri hiyo kwa muda mrefu amekuwa haridhishwi na utendaji kazi wa mhandisi huyo wa wilaya.