Mmoja afariki, 10 wajeruhiwa kwa ajali Arusha

Arusha.  Mwanajeshi mmoja,  MT 101414 George Ngwegeta amefariki katika ajali iliyotokea leo (Jumamosi) jioni katika kijiji cha Oldonyosambu wilayani Arumeru, huku abiria wengine 10 wakijeruhiwa.

Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amesema mwanajeshi huyo pamoja na majeruhi hao, walikuwa wamepanda gari dogo la abiria wakitoka Namanga kuelekea Arusha.

Amesema gari hilo lilipinduka mara tatu baada ya kupasuka tairi la mbele likiwa katika mwendo  kasi na dereva wa gari hilo,Pailoti Pamphili alishindwa kulidhibiti.

Mkumbo amesema majeruhi hao wamelazwa  katika hospitali ya Selian na Mount Meru huku jeshi la polisi likimshikilia dereva wa gari hilo aina ya Nissan Calavan, ambalo hufanya safari za Arusha- Namanga.