Mnara wa Lucky Vicent kuzinduliwa leo

Muktasari:

Wanafunzi walionusurika pia watakuwa miongoni mwa watu watakaohudhuria uzinduzi wa huo Mnara wa Lucky Vicent kuzinduliwa leo.


Arusha. Wanafunzi wa Shule ya Lucky Vincent waliorejea jana nchi kutoka Marekani watafika shuleni kwao leo.

Pia kutafanyika uzinduzi wa mnara wa kumbukumbu ya vifo vya wanafunzi 32,walimu wawili na dereva mmoja vilivyotokea Mei mwaka huu.

Wanafunzi ambao walinusurika na kupelekewa kwa matibabu nchini Marekani waliorejea jana  ni Doreen mshana,Sadia Awadh na Wilson Tarimo