Mongella: Msinialike kukagua miradi mibovu

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella 

Muktasari:

Badala yake amewaagiza kuwasimamia kwa karibu wakuu wa idara na wote wanaotekeleza miradi hiyo kuhakikisha inalingana na thamani ya fedha za umma zinazotumika.

Kwimba. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amewapiga marufuku viongozi na watendaji wa Serikali na halmashauri za wilaya mkoani humo kumwalika kutembelea au kukagua miradi iliyotekelezwa chini ya kiwango.

Badala yake amewaagiza kuwasimamia kwa karibu wakuu wa idara na wote wanaotekeleza miradi hiyo kuhakikisha inalingana na thamani ya fedha za umma zinazotumika.

Akizungumza na viongozi na watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Kwimba juzi, Mongella alitishia kuchukua hatua za kinidhamu na kisheria dhidi ya watendaji watakaoshindwa kusimamia miradi ya maendeleo, huku akitishia kuwahamishia ofisini kwake ili wapangiwe kazi nyingine.