Mtendaji wa kijiji auawa kwa kupigwa risasi

Muktasari:

Shuhuda wa tukio hilo, Dk Abdul Msemo ambaye ni mganga wa zahanati iliyopo kijijini hapo, alisema tukio hilo lilitokea saa 2:10 usiku wa kuamkia jana nyumbani kwa marehemu.

Kibiti. Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Nyambunda wilayani Kibiti, Ally Milandu ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi akiwa nyumbani kwake.

Shuhuda wa tukio hilo, Dk Abdul Msemo ambaye ni mganga wa zahanati iliyopo kijijini hapo, alisema tukio hilo lilitokea saa 2:10 usiku wa kuamkia jana nyumbani kwa marehemu.

Alisema wakiwa wanajadiliana mambo mbalimbali nyumbani kwa mtendaji, ghafla walifika watu watatu waliokuwa wamepanda pikipiki, mmoja alitoa bunduki aliyokuwa ameificha mgongoni mwake na kumpiga risasi tatu mtendaji  aliyefariki dunia papo hapo.