VIDEO: Muhimbili yampokea Mbowe

Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe 

Muktasari:

Mbowe anadaiwa kuanguka ghafla akiwa nyumbani kwake

Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Aminiel Aligaesha amesema Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe alipokelewa hospitalini hapo leo asubuhi.

Akizungumza na MCL Digital leo Juni 18, Aligaesha amesema: “Ni kweli tumempokea Mbowe leo asubuhi.”

Awali, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilielezwa kuwa, Mbowe ameshindwa kufika mahakamani baada ya kuanguka ghafla akiwa nyumbani kwake.

Wakili wake, Jeremiah Mtobesya aliiambia Mahakama leo kuwa mteja wake ameshindwa kufika mahakamani baada ya kuanguka ghafla nyumbani kwake.

Mkurugenzi wa Itifaki na Mawasiliano wa Chadema, John Mrema alisema ni kweli Mbowe ameanguka ghafla na amepelekwa Muhimbili.