Mungai afariki dunia

Aliyekuwa Waziri wa Elimu, Joseph Mungai wakati wa uhai wake

Muktasari:

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Aminiel Aligaesha amethibitisha kupokea Mungai akiwa bado mjonjwa na kumpeleka katika idara ya wagonjwa mahututi kabla ya kufikwa na mauti saa 11.20 jioni.

Dar es Salaam. Aliyekuwa Waziri wa Elimu, Joseph Mungai amefariki dunia leo (Jumanne) jioni.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Aminiel Aligaesha amethibitisha kupokea Mungai akiwa bado mjonjwa na kumpeleka katika idara ya wagonjwa mahututi kabla ya kufikwa na mauti saa 11.20 jioni.

Marehemu mbali na kuwa waziri wa elimu aliwahi kushika nyadhfa mbalimbali serikalini.