Muswada kuwezesha mikopo kwa wanafunzi waandaliwa

Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako

Muktasari:

 Waziri wa wizara hiyo, Profesa Joyce Ndalichako amesema Serikali imejiridhisha kuwa kozi zenye umuhimu na kipaumbele kwa Taifa lazima zipewe msukumo na kuwafanya vijana wasome zaidi, wakiwamo wahandisi.

Dodoma. Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria imeelezwa kuwa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi imeandaa pendekezo la muswada wa sheria kuwezesha mikopo kutolewa kwa wanafunzi wa Stashahada (Diploma) kwa kozi zenye kipaumbele kwa Taifa.
 Waziri wa wizara hiyo, Profesa Joyce Ndalichako amesema Serikali imejiridhisha kuwa kozi zenye umuhimu na kipaumbele kwa Taifa lazima zipewe msukumo na kuwafanya vijana wasome zaidi, wakiwamo wahandisi.
Amesema sehemu ya tatu ya pendekezo la muswada huo inapendekeza Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Sura ya 2004 kuchukua kozi za Stashahada na kuziingiza kwenye bodi hiyo.