Mvua kubwa kunyesha mikoa mitano kuanzia leo

Muktasari:

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema kuanzia leo Ijumaa Novemva 2 hadi 4, 2018 mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Kigoma, Mara na Katavi inatarajiwa kukubwa na mvua kubwa

Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhali ya kunyesha vipindi vya mvua kubwa kwa siku tatu na kutoa tahadhari kwa mikoa husika kuchukua

Taarifa ya TMA iliyotolewa leo Ijumaa Novemba 2,2018 imeitaja mikoa inayotarajia  kukubwa na mvua hizo ni Kagera, Geita, Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Kigoma, Mara na Katavi.

TMA imesema mvua hizo zinatarajiwa kuanza kunyesha leo hadi Novemba 4, 2018.

Imesema mvua hizo zinaweza kuleta athari ikiwemo kutokea mafuriko katika mitaa na kusababisha msongamano wa magari hasa katika maeneo ya mjini.

TMA imewataka wakazi wanaoishi maeneo hayo kuchukua tahadhari na kuendelea kufuatilia taarifa.