Mwalimu kizimbani kwa kubaka

Muktasari:

Amefikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Serengeti

 


Serengeti. Mwalimu wa shule ya sekondari Machochwe wilayani Serengeti Mkoa wa Mara, Peter Manko (28) amefikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Serengeti kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa kidato cha kwanza mwenye umri wa miaka 17.

Leo Agosti 21,2018 mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo, Ismael Ngaile, mwalimu huyo amesomewa mashtaka hayo namba 214/2018 na  mwendesha mashitaka wa Polisi,  Renatus Zakeo.

Zakeo amesema mwalimu huyo alitenda kosa hilo kati ya Januari 24 na Julai 9, 2018.

Amesema kitendo hicho ni kinyume na kifungu namba 130(1) na (2), (c) na 131(1) cha kanuni ya adhabu sura namba 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Mshitakiwa huyo amekana shitaka hilo  na kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 21, 2018 itakapotajwa tena. Mshakiwa huyo yupo nje kwa dhamana.