Nuru the Light huyu hapa...

Muktasari:

Nuru The Light ndilo jina analofahamika kisanii lakini jina lake kamili ni Nuru Magram ambapo anafafanua kuwa maisha yake kwa asilimia kubwa yapo Sweden.

“Muhogo Andazi” ndiyo ngoma yake inayofahamika zaidi, ikiwa ni kolabo ya mwanadada Nuru akimshirikisha bosi wa “Sharobaro Records” pia mwanamuziki Bob Junior.

Lakini kuna ngoma kadhaa kama Msela, Wewe, Walimwengu, Nisubiri Usilale na sasa ngoma ambayo inatamba inakwenda kwa jina la “Umeniacha”.

Nuru The Light ndilo jina analofahamika kisanii lakini jina lake kamili ni Nuru Magram ambapo anafafanua kuwa maisha yake kwa asilimia kubwa yapo Sweden.

“Kiukweli maisha yangu kwa asilimia kubwa yapo Sweden na hata mambo yangu mengi ninayoyafanya yapo kule lakini hapa Bongo pia ni Nyumbani na ninapapenda sana,” anasema.

Anaelezea wimbo wa “Umeniacha”

“Wimbo “Umeniacha” niliandika kwa sababu ni kitu kilichonitokea, Niliachwa na mpenzi wangu kwa hiyo niliumia lakini badae nikawa fresh na nikaona hii kitu kuna watu wengi huwa inawatokea lakini mimi niliishinda mapema,”

“Unajua watu wengi wanapoachwa hujiona kama wana matatizo lakini nimefanya huu wimbo kuonyesha kuwa kuachwa ni kitu cha kawaida alafu kwa huku Bongo mtu kuachwa yani huwa watu wengine wanafurahi kweli jambo ambalo si zuri.” anaongeza.

Sababu ya kuwa kimya kwa muda mrefu.

Anafafanua kuwa, sababu ya yeye kuwa kimya ni uamuzi wa kufanya mambo mengine hasa baada ya kuona sanaa ilianza kumletea matatizo kadhaa.

“Unajua mwanamke kutoka kimuziki ni kazi sana, kuna mambo mengi sana yani unakuta mtu anatamani kufanya kitu fulani kwasababu wewe unataka kitu fulani,”

“Alafu pia niliona kuna mambo yanatokea kama watu fulani wameamua kunifanyia hayo mambo sitaki kuyaweka sana wazi lakini sikupenda ndio maana nikaamua kukaa kimya, lakini nimegundua watu wengi sana walinimiss na nilifanya kosa kubwa sana kukaa kimya hivyo nimeamua kurudi tena ,” Aliongeza.

Maoni yake kuhusu muziki wa sasa na zamani

“Kwa mimi naona muziki haubadiriki lakini watu ndio wanaobadilika na pia mashabiki wanabadirika, mfano shabiki wangu aliyesikiliza “Muhogo Andazi” na sasa ni tofauti sana sababu umri umeongezeka na sifikiri kama vitu alivyokuwa anapenda kipindi hicho hakipo sawa na sasa,”

“Kwa hiyo muziki ni ule ule lakini watu ndio wanaobadilika na kuufanya muziki kuonekana mpya na mashabiki pia hivyo hivyo,” aliongeza.

Wasanii anaowakubali

“Mimi nampenda sana Barnaba, Angel Bernard, Remmy Ongala, Goodluck Gozbert na pia Msaga Sumu napenda sana kusikiliza nyimbo zao,”

“Natamani sana kufanya kolabo na Msaga Sumu, sababu nafikiri atanipa changamoto, muziki wake uko tofauti kwa hiyo itabidi kuna vitu atanielekeza sana kwahiyo nitafurahi sana kufanya nae kolabo,”

Kitu ambacho hawezi kusahau.

“Nakumbuka wakati tunaandaa wimbo wa Muhogo Andazi, siku ya kwanza umeme ulikatika kurudi siku ya pili kompyuta ikazingua na pia wakati tunashuti video hatukulala siku nzima na kama kazi ngumu inalipa baada ya kuachia tu wimbo ulipokelewa vyema sana,”

“Nilichogundua Watanzania tunapenda tumaneno neno twenye tafsida za chumbani chumbani ndio maana ulipendwa sana na hata pia tuliimba vyema sana kiukweli,” aliongeza.

Anamkumbuka Marehemu Albert Mangwair.

Anafafanua kuwa anamkumbuka sana Ngwair kwa sababu alifanya nae ngoma lakini haikuifanya vizuri sana. “Nilikuwa tena nakumbuka nataka kufanya nae video lakini sikua sana Serious sana na kila nikikutana nae alikuwa ananambia kuwa Nuru hautaki kufanya name kazi, Namimi nilikuwa namtania mara kwa mara lakini Ya Mungu mengi,”

“Mara ya mwisho namkumbuka nilikutana nae na akanambia kuwa ana taka kuongea nami na nilijua kuwa anataka kunambia nini lakini tulishindwa kukutana nikawa narudi, namkumbuka sana,”

Mipango ya albamu

“Albamu nipo naandaa nafikiri kufikia mwakani itakuwa tayari, hivyo mashabiki zangu wajiandae kupata vitu bora kwangu na katika albamu yangu mpya,” aliongeza.