Omotola atimiza miaka 40, afanya sherehe siku nne mfululizo

Muktasari:

Mbali na wanawake wenye uhitaji, Omotola aliwatembelea watoto yatima na kuwapatia zawadi mbalimbali.


Mwigizaji wa Nigeria, Omotola Jalade amefanya sherehe siku nne mfululizo akisherekea kutimiza miaka 40. Omotola aliyeingia katika uigizaji mwaka 1995 na filamu ya kwanza iliyoongozwa na Reginald Ebere, Venom Justice katika siku hizo nne amekutana na wanawake mbalimbali wenye uhitaji na kula nao pamoja.

Mbali na wanawake wenye uhitaji, Omotola aliwatembelea watoto yatima na kuwapatia zawadi mbalimbali.

Ni mwanamke anayejulikana kwa umahiri wake wa kucheza filamu, mwanaharakati, mwanamuziki na mwanamitindo.

Mara kadhaa jina lake limepamba vichwa vya habari, picha zake zimependezesha kurasa za majarida mengi duniani.

Mambo ambayo hukuyafahamu kuhusu Omotola

•Aliingia katika uigizaji kwa bahati mbaya. Alimsindikiza rafiki yake katika usaili wa kucheza filamu lakini kwa bahati mbaya alikosa na kumshawishi Omotola ajaribu akafanikiwa.

•Katika filamu yake ya kwanza alilipwa Naira 43,000 ambazo ni wastani wa Sh304,000 za Tanzania.

•Pamoja na kuwa ameolewa huwa anatongozwa na wanaume mbalimbali na kwamba alishawahi kushawishika lakini aliyashinda majaribu hayo.

Marafiki zake wa karibu ni pamoja na Rita

Dominic, Omoni Oboli, Rukky Sanda, Zeb Ejiro, na Chidi Mokeme.

•Filamu ambayo anaamini ilimtambulisha

vyema ni My Story.

•Vitu anavyovichukua katika uigizaji ni kucheza scene za chumbani.