Pengo kurudi tena India kwa matibabu

Askofu Mkuu wa Jimbo la Dar es Salaam,Kardinali  Polycarp Pengo

Muktasari:

Mnamo mwezi Januari mwaka huu,Askofu  Pengo alilazwa katika hospitali ya Muhimbili(MNH) kutokana na hali yake kiafya kutokuwa nzuri licha ya Ugonjwa unaomsumbua kutowekwa wazi.

Dar es Salaam.Hali ya kiafya ya Askofu Mkuu wa Jimbo la Dar es Salaam,Kardinali  Polycarp Pengo imeendelea kutetereka hali inayomlazimu kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu zaidi.
Mnamo mwezi Januari mwaka huu,Askofu  Pengo alilazwa katika hospitali ya Muhimbili(MNH) kutokana na hali yake kiafya kutokuwa nzuri licha ya Ugonjwa unaomsumbua kutowekwa wazi.
Kardinali Pengo alilazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ambapo baadhi ya Viongozi wa nchi walimtembelea akiwamo Rais John Magufuli.
Akizungumza wakati wa Ibada iliyofanyika leo(ijumaa) katika Parokia ya Mbagala Askofu Pengo amesema analazimika kwenda nchini India kwa matIbabu zaidi.
"Oktoba 23 natarajia kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu kwa kuwa hali yangu kiafya sio nzuri hivi sasa",amesema.
Katika Ibada hiyo kulifanyika harambee kwa ajili ya kuchangia Kituo cha Malezi ya wadada Wadogo(Masista) Cha Mbagala ambapo zaidi ya Milioni 142 zilipatikana.