Wednesday, August 3, 2016

Picha za mke wa Trump akiwa mtupu zaanikwa

Melania, mke wa bilionea na mgombea Urais

Melania, mke wa bilionea na mgombea Urais nchini Marekani, Donald Trump 

Washington. Hali imezidi kuwa ngumu kwa mgombea urais wa Marekani, Donald Trump wa Chama cha Republican baada ya mke wake kumtia doa kwa kuonekana picha zake za utupu.

Picha hizo zilianikwa kwenye jarida la New York Post la Marekani Julai 13 mwaka huu na kuwa gumzo mitandaoni. Pia, inaelezwa huenda zikamdhoofisha Trump na kumshushia heshima ndani na nje ya nchi yake.

Ikiwa imebaki miezi mitatu Wamarekani wafanye Uchaguzi Mkuu, juzi  Kituo  cha Habari cha CNN kilifanya mahojiano na mshauri mkuu wa mgombea huyo, Jason Miller na kusema picha hizo za Melania zina miaka 20 kabla mwanamke huyo hajafahamiana na Trump.

“Siyo jambo la kushangaza Melania ni mwanamke mrembo hakuna ubishi katika hilo,” amesema  Miller.

 

-->