Pluijm aacha wasia kwa wachezaji Yanga

Muktasari:

Pluijm alitangaza kujiuzulu nafasi hiyo juzi, baada ya klabu hiyo kumleta nchini kocha  mpya, raia wa Zambia, George Lwandamina aliyesaini mkataba wa miaka miwili.

Dar es Salaam. Kocha Hans Pluijm  akiwaaga wachezaji wa Yanga jana wakiwa mazoezini amesema anatamani kuiona klabu hiyo ikitwaa ubingwa.

Pluijm alitangaza kujiuzulu nafasi hiyo juzi, baada ya klabu hiyo kumleta nchini kocha  mpya, raia wa Zambia, George Lwandamina aliyesaini mkataba wa miaka miwili.

Wakati wa mazoezi yaliyofanyika Uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini, Dar es Salaam, Pluijm aliwaambia wachezaji kuwa atawakumbuka, lakini wanatakiwa kupendana na kutanguliza mbele masilahi ya timu.