Rais Magufuli afanya uteuzi mwingine

File Photo

Muktasari:

Taarifa iliyoletwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu, imeeleza kuwa Ole Sendeka anachukua nafasi ya Dk Rehema Nchimbi ambaye amehamishwa kituo cha kazi na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.

Dar es Salaam.  Rais John Magufuli amemteua Dk Osward J. Mashindano kuwa Msajili wa Hazina nafasi aliyokuwa nayo Lawrence Mafuru ambaye atapangiwa kazi nyingine; pia amemteua Christopher Ole Sendeka kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe.

Taarifa iliyoletwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu, imeeleza kuwa Ole Sendeka anachukua nafasi ya Dk Rehema Nchimbi ambaye amehamishwa kituo cha kazi na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.

Nchimbi anajaza nafasi iliyoachwa na Mhandisi Mathew Mtigumwe ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo anayeshughulikia Kilimo.

Pamoja na mabadiliko hayo ya Singida, kadhalika Rais amefanya mabadiliko madogo katika Wizara na Mikoa kama ifuatavyo.

Amemteua Profesa Faustin Kamuzora kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais. Profesa Kamuzora alikuwa Katibu Mkuu Mawasiliano.

Kadhalika Rais amemteua Mhandisi Mathew Mtigumwe kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo anayeshughulikia Kilimo. Mtigumwe anachukua nafasi ya Dk Frolence Turuka ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Kabla ya uteuzi huo Turuka alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi aliyekuwa akishughulikia Kilimo. Anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Job Masima ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.

Pmamoja na Turuka, Rais Magufuli amemteua Dk Maria Sasabo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano atakayeshughulikia Mawasiliano.

Dk Sasabo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Profesa Kamuzora ambaye ameteuliwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais.

Wengine walioteulwia ni Mhandisi Angelina Madete anayekuwa Naibu Katibu Mkuu Katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Madete anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk Sasabo.

Aloyce K. Nzuki ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii.