Rais Magufuli ateua Kamishna wa Polisi Zanzibar

Muktasari:

Kabla ya uteuzi huu Kamishna Haji alikuwa mhasibu mkuu wa Polisi Zanzibar

Taarifa iliyotolewa leo Februari 10, 2018 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imesema kuwa Rais amempandisha cheo Haji kutoka Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) na kuwa Kamishna wa Polisi (CP), na kisha kumteua kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar. Uteuzi huo umeanza leo.

Kabla ya uteuzi huu Kamishna Haji alikuwa mhasibu mkuu wa Polisi Zanzibar. Kamishna huyo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna wa Polisi Hamad Omar Makame ambaye amestaafu.