Ras aikwepa kamati ya hesabu

Meya wa Jiji la Dar, Isaya Mwita

Muktasari:

Viongozi wa Jiji la Dar es Salaam wakiongozwa na Meya wa Jiji, Isaya Mwita na Mkurugenzi wake, Sipora Liana na wataalamu wengine walifika, lakini katibu tawala hakuwapo.

Dodoma. Katibu Tawala wa Mkoa (Ras),  Telesia Mbando ameshindwa kukutana na Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) ili kujibu maswali ya wajumbe.

 Viongozi wa Jiji la Dar es Salaam wakiongozwa na Meya wa Jiji, Isaya Mwita na Mkurugenzi wake, Sipora Liana na wataalamu wengine walifika, lakini katibu tawala hakuwapo.

 Wajumbe wa kamati walitaka maelezo ya kina aliko katibu tawala, lakini yalitolewa maelezo kuwa alipata udhuru na hivyo akamtuma mtu mwingine, ingawa hakuwa na barua.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati, Abdallah Chikota alikasirishwa na kitendo hicho akisema kulikuwa na maswali mengi ya Ras na kutokufika kwake ni dharau kwa kamati.