Rugimbana: Majengo yanahitaji kukarabatiwa

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana

Muktasari:

Amesema Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) umepewa jukumu la kuandaa makazi ili Serikali iweze kuhamia Dodoma kwa asilimia 70.

Dodoma. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana amesema Serikali inahamia mkoani hapa kwa awamu kutokana na baadhi ya majengo kuhitaji kukarabatiwa na mengine kumalizia ujenzi.

Amesema Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) umepewa jukumu la kuandaa makazi ili Serikali iweze kuhamia Dodoma kwa asilimia 70.

Rugimbana amesema jengo la ofisi yake ni miongoni mwa majengo yanayohitajika kumaliziwa na kwamba  ujenzi umefikia asilimia 70. Amesema ghorofa za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) nazo ujenzi umefikia asilimia 90.

“Kilichobakia kwenye majengo ya jeshi ni kuwekwa maji,  umeme na vitu vingine vya umaliziaji,” alisema.