Serikali kuteua maofisa wakaguzi mazingira 200

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira ),January Makamba

Muktasari:

Makamba ametoa kauli  hiyo leo wakati akizungumza na wananchi na viongozi wa wilayaya Korogwe mkoani Tanga  katika ukumbi wa halmashauri hiyo.

Korogwe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira ),January Makamba amesema Serikali hivi karibuni itawateua maofisa wakaguzi wa mazingira 200 kwa ajili ya kuongeza nguvu ya uhifadhi wa mazingira nchini.

Makamba ametoa kauli  hiyo leo wakati akizungumza na wananchi na viongozi wa wilayaya Korogwe mkoani Tanga  katika ukumbi wa halmashauri hiyo.

Makamba ameyasema hayo baada ya uongozi wa wilaya hiyo kumweleza kuwa bado wanakabiliwa na upungufu wa wakaguzi wa mazingira katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira halmashauri.

Amesema wakaguzi hao watapelekwa katika wilaya mbalimbali ikiwamo ya Korogwe na kwamba tayari majina yameshapatikana na wakaguzi hayo watapewa mafunzo kabla ya kusambazwa.