Serikali yakomalia matibabu bure kwa wazee

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu

Muktasari:

  • Yataka kadi za matibabu ya bure zitolewe haraka.

Dodoma. Serikali imezikumbusha halmashauri zote nchini kutoa kadi za matibabu ya bure kwa wazee ili kuwaondolea usumbufu wanaupata wanapohitaji huduma hiyo.

Agizo hilo lililotolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na kulisisitiza tena leo, Jumanne bungeni.

Waziri huyo alizitaka halmashauri ambazo bado hazijatekeleza agizo hilo kuiga mfano mxuri uliopo kwenye halmashauri za Kasulu, Shinyanga na Mbarali.

Alisisitiza kuharakishwa kwa suala hilo na kusema, "Sio kila Mara mzee anapotaka matibabu ahangaike kukamilisha taratibu."

Hata hivyo, Serikali inakamilisha taratibu na kutunga Sheria ya bima ya Afya kwa wote itakayozilazimu halmashauri kuwalipia wazee wote kadi za bima ya mfuko wa jamii (CHF).