Simulizi mauaji ya Kibiti

Muktasari:

Alisema Kubezya alifanikiwa kurejesha nidhamu kwa polisi waliokuwa wakijihusisha na vitendo vya unyanyasaji wa raia kama vya kuwakamata vijana wanaobeba mbao kwa ajili ya kujitafutia riziki  na kuwapora.

Dar/Pwani. Shuhuda wa tukio la mauaji ya Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kibiti, Peter Kubezya na maofisa wawili wa maliasili na utalii, Samwel Joseph amesema kifo hicho kimekatisha ndoto ya askari huyo kuhakikisha amani inatawala.

Alisema Kubezya alifanikiwa kurejesha nidhamu kwa polisi waliokuwa wakijihusisha na vitendo vya unyanyasaji wa raia kama vya kuwakamata vijana wanaobeba mbao kwa ajili ya kujitafutia riziki  na kuwapora.

“Tumepoteza mpambanaji aliyelenga kuutokomeza ujambazi wilayani hapa unaozidi kuota mizizi kila kukicha,” alisema.

Mkazi mwingine wa eneo hilo, Daudi Siang’a alisema: “Alikuwa amedhamiria hasa na ndiyo maana alijitoa kimasomaso kukabiliana na majambazi.”

Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, WP Jesca, kutoka ofisi ya habari ya polisi mkoani Pwani, alisema wanaendelea na uchunguzi ili kuwatia mbaroni waliohusika katika mauaji hayo.