Sumaye apamba uzinduzi kampeni za ubunge Ukonga

Muktasari:

Asia Msangi anawania ubunge jimbo la Ukonga kupitia Chadema

Dar es Salaam. Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye ni miongoni mwa viongozi wa Chadema walioshiriki uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Ukonga leo Jumamosi Agosti 25, 2018.

Uchaguzi huo utafanyika Septemba 16, 2018  baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Mwita Waitara  kwa tiketi ya Chadema, kujiuzulu na kuhamia CCM ambako ameteuliwa kuwania tena ubunge katika jimbo hilo.

Baadhi ya viongozi wa Chadema waliohudhuria uzinduzi huo ni mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Salum Mwalimu.