TCB yakosa uongozi wa juu

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba

Muktasari:

Taarifa zilizopatikana jana zinasema bodi ya wakurugenzi iliyokuwapo chini ya Mwenyekiti, Dk Juma Ngasongwa ilimaliza muda wa uongozi Februari mwaka jana.

Moshi. Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB) yenye makao makuu mjini hapa, haina bodi ya wakurugenzi wala mkurugenzi mkuu kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.

Taarifa zilizopatikana jana zinasema bodi ya wakurugenzi iliyokuwapo chini ya Mwenyekiti, Dk Juma Ngasongwa ilimaliza muda wa uongozi Februari mwaka jana.

Mbali na bodi kumaliza muda wake, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TCB, Injinia Adolf Kumburu alistaafu Septemba 15, 2015 baada ya mkataba kumalizika. Tangu wakati huo, mamlaka zenye dhamana ya uteuzi wa viongozi hao hazijateua.

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba alipoulizwa na gazeti hili jana alisema kutokuwapo kwa bodi ya wakurugenzi na mkurugenzi mkuu kumeathiri baadhi ya uamuzi.