TacRi yagundua miche mipya ya kahawa

Muktasari:

Akizungumza mjini hapa, Mtenga amesema katika utafiti huo pia wamezingatia mbegu ambazo zinavumilia ukame na zile zinazovumilia magonjwa yatokanayo na mazingira ya kilimo cha zao hilo hapa nchini

Hai. Mtafiti mwandamizi wa Taasisi ya Utafiti wa Kahawa (TacRi), Dk Damian Mtenga amesema wako katika hatua za mwisho za kukamilisha utafiti wa miche inayovumilia ukame itakayotumika kuanzia msimu wa kilimo wa  2018/2019.

Akizungumza mjini hapa, Mtenga amesema katika utafiti huo pia wamezingatia mbegu ambazo zinavumilia ukame na zile zinazovumilia magonjwa yatokanayo na mazingira ya kilimo cha zao hilo hapa nchini.

Katika hatua nyingine, mkutano mkuu wa tisa wa TaCRI umemchagua mjumbe wa bodi hiyo kutoka mkoani Mbeya, Aloyce Msangawale kuwa mwenyekiti.

Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Vedasto Ngaiza amesema Msangawale ambaye ni mkulima anachukua nafasi yake kuanzia sasa.

Ngaiza amesema katika kipindi cha miaka 15, taasisi hiyo imepata mafanikio makubwa ikiwamo kugundua aina 23 mpya za miche ya kahawa za Arabika na Robusta zinazovumilia magonjwa.

“Katika ugunduzi huu, aina 19 zilikuwa ni za Arabika na nne za Robusta ambazo huzaa kwa wingi, hili litawasaidia wakulima kupata mazao mengi,” amesema Ngaiza.