Tanzania, China zasaini mkataba wa utamaduni

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye

Muktasari:

Waziri Nape ameeleza kuwa Mkataba huo una lengo la kuimarisha  na kuendeleza ushirikiano katika Sekta ya Utamaduni ambao umedumu kwa miaka mingi ulioasisiwa na Baba wa Taifa Julius K. Nyerere.

Dar es Salaam. Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye pamoja na Naibu Waziri wa Utamaduni kutoka Jamhuri ya  watu wa China  Dong Wei wamesaini programu ya utekelezaji wa Mkataba wa masuala ya Utamaduni wa miaka mitatu kuanzia mwaka 2017 hadi 2020 leo Jijini Dar es Salaam.

Waziri Nape ameeleza kuwa Mkataba huo una lengo la kuimarisha  na kuendeleza ushirikiano katika Sekta ya Utamaduni ambao umedumu kwa miaka mingi ulioasisiwa na Baba wa Taifa Julius K. Nyerere.

“Tanzania na China tumekuwa na ushirikiano wa muda mrefu wa masuala mbalimbali ikiwemo hili la Utamaduni ambalo limetumika kukuza, kulinda na kuunganisha nchi zetu kuwa kitu kimoja”, Alisema Nape

Kwa upande wake Waziri Wei amesema ushirikiano kati ya Tanzania na China ulikuwepo kwa muda mrefu  katika masuala  ya Utamaduni, Sanaa, Elimu,Ngoma na  Michezo.

 “Ushirikiano wetu wa muda mrefu katika  masuala ya Utamaduni umeleta mafanikio makubwa ambayo sote tunajivunia kila tunapokuwa pamoja”.Alisema  Wei