Tanzania mpokeaji mkubwa misaada ya Japan

Mwakilishi Mkuu wa Jica, Toshio Nagase

Muktasari:

Jica wamekuwa wakifanya shughuli mbalimbali za kimaendeleo kwa Tanzania kama ilivyo kwa nchi nyingine za Kusini mwa Jangwa la Sahara. 

Dar es Salaam. Tanzania imeshika nafasi ya tatu kati ya wapokeaji wakubwa wa misaada ya Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (Jica) miongoni mwa nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa mwaka 2015.

Mwakilishi Mkuu wa Jica, Toshio Nagase, amesema kiwango cha upokeaji wa misaada nchini kilifikia Sh 235 bilioni kati ya Sh 3trilioni kwa nchi za Kusini mwa Sahara.

Nagase amesema Tanzania inafuatiwa na Kenya ambapo imepata msaada wa Dola 249, 88 milioni na Angola Dola 220.55 milioni.

"Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD), Japan ilitoa Dola 94.84 za misaada ya rasmi ya Maendeleo (ODA) kwa Tanzania," amesema Nagase.

Nagase amesema mwaka 2106/2017, Jica wamefanya shughuli mbalimbali ikiwemo ujenzi wa barabara ya juu (flyover) eneo la Tazara ambayo ni ya kwanza katika historia ya Tanzania.