Tanzania yajipanga kuvuna Cuba

Waziri wa Mambo ya Nje, Dk Augustine Mahiga

Muktasari:

Mesa atafanya ziara ya siku tatu nchini ambayo ni kiashirio cha ushirikiano wa nchi hizo uliodumu kwa zaidi ya miaka 50 sasa.

Dar es Salaam. Wakati Makamu wa Rais wa Cuba, Salvador Antonio Valdes Mesa akitarajiwa kuwasili nchini kesho, Serikali imepanga kuimarisha ushirikiano na nchi hiyo katika sekta za uwekezaji, biashara, kilimo na viwanda.

Mesa atafanya ziara ya siku tatu nchini ambayo ni kiashirio cha ushirikiano wa nchi hizo uliodumu kwa zaidi ya miaka 50 sasa.

Akizungumzia ziara hiyo jana jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk Augustine Mahiga alisema ziara hiyo ni muhimu kwa sababu itafungua milango mipya ya uwekezaji, kilimo, biashara na viwanda.

Alisema ushirikiano wa Tanzania na Cuba uliasisiwa na Mwalimu Julius Nyerere na aliyekuwa Rais wa Cuba, Fidel Castro.