Top100 pasua kichwa Kanda ya Ziwa

Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Ltd (MCL), Francis Nanai .Picha ya Maktaba

Muktasari:

  • Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo mkoani hapa jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Ltd (MCL), Francis Nanai alisema ushiriki wa mikoa ya Kanda ya Ziwa ni mdogo ukilinganisha na Dar es Salaam

Mwanza. Licha ya mashindano ya Kampuni 100 bora za kiwango cha kati (Top 100) kuanzishwa miaka mitano iliyopita, ushiriki wa mikoa ya Kanda ya Ziwa umeendelea kusuasua.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo mkoani hapa jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Ltd (MCL), Francis Nanai alisema ushiriki wa mikoa ya Kanda ya Ziwa ni mdogo ukilinganisha na Dar es Salaam

 “Tungependa kuona ushiriki mkubwa kutoka mikoani, hasa Kanda ya Ziwa ambayo ni kiunganishi cha biashara katika ukanda huu wa Mataifa ya Afrika Mashariki na Maziwa Mkuu,” alisema Nanai.

Meneja wa Fedha na Utafiti wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) ambaye pia ni miongoni mwa wawezeshaji kutoka taasisi ya utafiti na ukaguzi ya KPGM, Ibrahim Mshindo alisema changamoto kubwa wanayokumbana nayo ni uelewa mdogo na woga miongoni mwa wafanyabiashara katika kushiriki mambo mapya.