UDSM, Waholanzi wabadilishana uzoefu

Shule Kuu ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS)

Muktasari:

Mhadhiri Msaidizi wa UDBS, David Rweikiza amesema mafunzo hayo yanawaongezea wanafunzi uelewa na kuwaza fursa zinazowazunguka.

Dar es Salaam. Shule Kuu ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS), inaendesha kongamano la kubadilishana uzoefu wa mafunzo kwa wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya Uholanzi na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ili kukuza mawazo ya wanafunzi kujiajiri katika sekta ya viwanda.

Mhadhiri Msaidizi wa UDBS, David Rweikiza amesema mafunzo hayo yanawaongezea wanafunzi uelewa na kuwaza fursa zinazowazunguka.

Rweikiza amesema wakimaliza mafunzo ya nadharia na kwenda kufanya kwa vitendo, watafikiria jinsi ya kuwekeza.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Hanze Applied Sciences nchini Uholanzi, Paul Wabike amesema hiyo ni mara yao ya kwanza kushiriki kongamano hilo na kwamba, hivi sasa wanawashauri wanafunzi kuwekeza kimataifa na kwenda nje zaidi ya mipaka.