Uber yanyimwa leseni ya usafirishaji

Muktasari:

  • Tfl imehitimisha kwa kusema kwamba kampuni hiyo inayowaunganisha abiria na madereva kwa teknolojia ya simu haifai kupewa leseni.

London, Uingereza. Kampuni maarufu ya usafirishaji abiria ya Uber imenyimwa leseni mpya kwa kazi hiyo jijini, Shirika la Usafiri la London (TfL) limesema.

TfL imehitimisha kwa kusema kwamba kampuni hiyo inayowaunganisha abiria na madereva kwa teknolojia ya simu haifai kupewa leseni kwa ajili ya kuendesha biashara ya kukodisha magari

Kampuni ya Uber inatumia programu ya simu ya mkononi, inatumia mfumo wa utambuzi wa eneo (GPS) kufahamu alipo abiria, muda, umbali na gharama halisi hadi anakokwenda abiria.

Shirika hilo la Usafiri limesema kuwa limechukua uamuzi huo kwa kuzingatia “masuala ya usalama na ulinzi”.

Ikithibitisha kwamba itakata rufani dhidi ya uamuzi huo, Uber imesema imeuonyesha ulimwengu “mbali ya kuwa wazi, London imefungia makampuni bunifu.”

Abiria wapatao 3.5 na madereva 40,000 wanatumia magari ya Uber ambayo hutumia mtandao jijini London.