Ukawa na CCM kutikisa majukwaa kwa siku 30

Muktasari:

Mbali na ubunge, mtifuano huo utafanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Singida, Mwanza, Dodoma, Iringa, Manyara, Mara, Arusha, Katavi, Ruvuma, Kagera, Shinyanga, Kilimanjaro, Simiyu na Pwani.

Dar es Salaam. Baada ya mwaka mzima wa Serikali kuzuia mikutano ya hadhara, vyama vya CCM,  Ukawa, ACT Wazalendo na vingine vinatarajiwa kuwasha moto kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Dimani, Zanzibar na madiwani katika kata 22 kwenye halmashauri 21 za Tanzania Bara kwa mwezi mzima.

Mbali na ubunge, mtifuano huo utafanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Singida, Mwanza, Dodoma, Iringa, Manyara, Mara, Arusha, Katavi, Ruvuma, Kagera, Shinyanga, Kilimanjaro, Simiyu na Pwani.

Uchaguzi huo unatarajiwa fursa ya kwanza kwa vyama vya siasa kupata uwanja wa kufanya mikutano ya hadhara kunadi sera zao na pengine kipimo cha utawala wa Rais John Magufuli katika uongozi wa Serikali na chama tawala.

Habari zaidi soma gazeti la Mwananchi