Ulyanhulu kuonja uchungu wa bomoabomoa

Picha ya Maktaba.

Muktasari:

  • Kaimu Mkuu wa Makazi ya Ulyankulu, Samwel Makungu alisema wote waliojenga nyumba za kudumu baada ya kupata uraia wa Tanzania, wamekiuka sheria kwa vile makazi hayo hayaruhusiwi.
  • “Sheria zipo wazi... hairuhusiwi kujengwa nyumba za kudumu na hatua zitachukuliwa dhidi ya waliokiuka,” alisema.

Kaliua. Waliokuwa wakimbizi ambao wamejenga makazi ya kudumu eneo la Ulyankulu wilayani Kaliua kinyume cha sheria, nyumba zao zitabomolewa na hawatalipwa fidia.

Kaimu Mkuu wa Makazi ya Ulyankulu, Samwel Makungu alisema wote waliojenga nyumba za kudumu baada ya kupata uraia wa Tanzania, wamekiuka sheria kwa vile makazi hayo hayaruhusiwi.

“Sheria zipo wazi... hairuhusiwi kujengwa nyumba za kudumu na hatua zitachukuliwa dhidi ya waliokiuka,” alisema.

Makungu alisema baadhi ya wakazi hao wamekuwa wakikaidi agizo la Serikali la kutojenga makazi ya kudumu eneo hilo.

Baadhi ya wakazi wa eneo hilo, walisema wanalipenda ndiyo maana wamejenga kwani hawaamini kama wataruhusiwa kuendelea kuishi hapo moja kwa moja.