Wachezaji wa soka

Muktasari:

Makamu wa Rais wa ZFA, Ali Mohamed Ali amesema  klabu nyingi zilijitokeza kuchukua fomu za usajili, lakini hadi wakati huu ni idadi ndogo tu ya fomu zilizorejeshwa katika ofisi yake.

Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) kimesema ukosefu wa fedha kwa klabu za visiwani hapa ni moja ya sababu ya  kudorora kwa usajili wa dirisha dogo.
Makamu wa Rais wa ZFA, Ali Mohamed Ali amesema  klabu nyingi zilijitokeza kuchukua fomu za usajili, lakini hadi wakati huu ni idadi ndogo tu ya fomu zilizorejeshwa katika ofisi yake.
Amesema viongozi wengi wa klabu walijitokeza kuchukua fomu hizo mwishoni mwa mzunguko wa kwanza.
“Uchukuaji wa fomu kwa klabu ulikuwa ni mkubwa na ulitufanya tuwe na imani kuwa mzunguuko wa pili utakuwa na upinzani mkali kwa kila timu, lakini kumbe ni kinyume chake,” amesema makamu huyo.
 kuanza mwisho mwa mwezi huu.