Uuzaji pamba wanasa vidagaa

Muktasari:

  • Washtakiwa katika kesi hiyo ni Annastazia Tagara (44), aliyenunua pamba na Salawa Ngelela (29) ambaye ni muuzaji.

Igunga. Bodi ya Pamba Tanzania (TCB) Wilaya ya Igunga mkoani Tabora kwa kushirikiana na polisi, imewafikisha mahakamani watu wawili kwa kosa la kuuza na kununua zao hilo chafu kinyume cha sheria.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni Annastazia Tagara (44), aliyenunua pamba na Salawa Ngelela (29) ambaye ni muuzaji.

Mwendesha mashtaka wa polisi, Elimajidi Kweyamba alidai jana kuwa, washtakiwa hao walitenda kosa hilo Julai 16 saa tano asubuhi Kijiji cha Isugilo.

Hata hivyo, washtakiwa kwa pamoja walikana mashtaka yao na wapo nje kwa dhamana ya Sh7 milioni kila mmoja hadi Julai 28, itakapotajwa tena.