VIDEO: Mkuu wa Wilaya ashauri wanawake kuacha kutumia vipodozi vyenye sumu

Muktasari:

Wanawake wametakiwa kuwa mabalozi wazuri wa kukemea watumiaji wa vipodozi vyenye sumu

Dar es Salaam. Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema amewataka wanawake, na jamii kwa ujumla nchini kuacha kutumia vipodozi vyenye  sumu ambavyo vitahatarisha afya zao na kuwataka kuwa mabalozi wazuri kukemea hali hiyo pale wanaponunua bidhaa hizo.
Mjema amesema hayo leo Novemba 18  wakati wa kuzindua kampeni ya Afya na Urembo iliyoandaliwa na Kampuni ya Timeless Saloon inayojihisisha na masuala mbalimbali na Urembo.
Amesema maisha ya wanawake yanaharibiwa na vipodozi ambavyo havijakidhi matakwa ya utumiaji na vingine vikiwa ni kwa ajili ya biashara jambo ambalo sio salama katika kipindi hiki cha kukuza uchumi wa kati na viwanda.
"Jambo hili ni zuri kwani kupitia kampeni hii wanawake kwa ujumla na hata wanaume wataweza kupata elimu bora ya kutumia vipodozi mbalimbali na kusaidia kupunguza athari kubwa zinazoendelea kuwanyemelea wanawake wengi ikiwemo kutoa harufu na kujibadilisha rangi yangu ngozi, "amesema  Mjema.
"Serikali inaendelea kupiga marufuku suala la kutumia vipodozi vyenye sumu na ambavyo havijakidhi vigezo hivyo niwaombe wanawake kukataa hali hiyo na kwa kufanya hivyo tunaweza kupiga hatua katika kujiajiri  wenyewe na kwa kutumia vitu asili kwa kutengeneza mafuta na vipodozi vingine, "amesema
Mbali na hilo Mjema alipongeza jitihada zilizofanywa na kampuni hiyo kwa kuwajali wanawake katika Urembo na ujasiriamali kiti ambacho serikali ya awamu ya tano katika kwa mkoa wa Dar es Salaam kumeanzishwa jukwaa la  wanawake wanajikomboa kiuchumi na kuwafikia na kuwatambua ili waweze kupatiwa msaada zaidi hasa.
Mkurugenzi wa Timeless Saloon, Irene Moshi amesema lengo la kuanzisha kampeni hiyo ni kulingana na matakwa ya wateja wake katika kuulizia masuala ya afya ikiwemo kunuka kwa kinywa, harufu mbaya ya mwili na ngozi.
"Mahitaji yalikuwa mengi katika kufahamu mambo ambayo yako nje katika masuala ya Urembo hivyo tukaamua kuungana na wadau mbalimbali wa afya ili kuendesha kampeni hii ili kusaidia jamii kwa ujumla, "amesema  Moshi.
Amesema katika kuhakikisha wanawake wanakuwa warembo lazima suala la afya lizingatiwe ili waweze kujishughulisha katika kukuza uchumi wa viwanda na wa kati.