Album ya Vanessa Mdee yagharimu zaidi ya Sh100 milioni

Muktasari:

Ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Januari 20 jijini Dar es Salaam wakati akiuza CD za albamu hiyo kwa wakazi wa jijini hapa waliojitokeza kwa wingi katika maduka ya Mlimani City. CD moja anauza kwa Sh10,000.

Dar es Salaam. Msanii wa muziki wa kizazi kipya,  Vanessa Mdee amesema ametumia zaidi ya Sh100 milioni kuandaa albamu yake ya Money Mondays yenye nyimbo 17.
Ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Januari 20 jijini Dar es Salaam wakati akiuza CD za albamu hiyo kwa wakazi wa jijini hapa waliojitokeza kwa wingi katika maduka ya Mlimani City. CD moja anauza kwa Sh10,000.
Amesema licha ya baadhi ya watu kudai ametumia kiasi kikubwa cha fedha  kuandaa album hiyo, haoni kama ni sawa kusema hivyo kwa maelezo kuwa muziki unahitaji uwekezaji mkubwa.
“Baada ya kuuza CD hizi Dar es Salaam nitakwenda mikoa mbalimbali ili kuwafikia mashabiki wangu japo kwa sasa kuna mawakala wanaendelea kuuza CD zangu huko mikoani,” amesema Vanessa.