Vodacom yawachangia Mundindi Sh15 milioni

Muktasari:

Msaada huo unaojumuisha vyakula, sabuni, magodoro na mablanketi ulikabidhiwa na Meneja wa Vodacom mkoani Njombe, Benedict Kitogwa kwenye shule hiyo iliyopo wilayani Ludewa. “Sisi ni sehemu ya jamii hivyo ni lazima tushirikiane na makundi yote. Kuwajali watu wenye mahitaji maalumu. Ni jukumu la jamii nzima,” alisema Kitogwa.

Njombe. Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom imetoa Sh15 kuchangia Shule Maalumu ya Msingi ya Mundindi ya watoto wenye ulemavu.

Msaada huo unaojumuisha vyakula, sabuni, magodoro na mablanketi ulikabidhiwa na Meneja wa Vodacom mkoani Njombe, Benedict Kitogwa kwenye shule hiyo iliyopo wilayani Ludewa. “Sisi ni sehemu ya jamii hivyo ni lazima tushirikiane na makundi yote. Kuwajali watu wenye mahitaji maalumu. Ni jukumu la jamii nzima,” alisema Kitogwa.

Uongozi wa shule hiyo uliishukuru Vodacom kwa msaada huo na kuwataka wadau wengine kujitokeza kuchangia mahitaji ya watoto hao ili kufanikisha elimu yao.